Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Serikali Kushindanisha Wawekezaji sekta ya Nishati

Serikali Kushindanisha Wawekezaji sekta ya Nishati

Picha
Na Veronica Simba-Maelezo Serikali imesema ushindani kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika sekta ya nishati, ndiyo njia bora zaidi itakayowezesha kuwapata wawekezaji wenye vigezo vinavyotakiwa. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aliyasema hayo jana, Mei 10, alipokutana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KOYO kutoka Japan, Norio Shoji na Ujumbe wake, ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika uzalishaji na usafirishaji wa umeme nchini, kwa kutumia vyanzo mbalimbali ikiwemo gesi asilia na jua. “Kampuni nyingi zimeonesha nia ya kuwekeza kwenye sekta ya nishati. Serikali inao uhitaji mkubwa wa wawekezaji walio makini, hivyo tunahitaji kuwapata wawekezaji wenye vigezo kwa kutumia ushindani unaozingatia uwazi,” alisisitiza Profesa Muhongo. Aliongeza kuwa, ili kuwarahisishia wawekezaji wenye nia ya kuwekeza katika sekta ya nishati nchini, Wizara inaandaa taarifa maalum itakayobainisha maeneo yanayohitaji uwekezaji pamoja na vipaumbele vyake. Alisema, taarifa h...