Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Polisi Dar Yakamata Ombaomba 45 Dar

Polisi Dar Yakamata Ombaomba 45 Dar, 17 Wapelekwa gerezani

Picha
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, wamewakamata na kuwaondoa ombaomba 45 na 17 wamewapeleka gerezani.    Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema jana kuwa jeshi hilo kwa kushirikiana na Idara ya Ustawi wa Jamii, wanafanya utaratibu wa kuhakikisha watu hao wanarudishwa mikoani walikotoka.    “Kazi hii inaenda vizuri na ombaomba wachache wamebakia ambao wakiwaona askari wanakimbia na kutokomea kusikojulikana,” alisema Sirro.  Katika tukio lingine, Polisi wanawashikilia watuhumiwa 96 wenye umri wa miaka 15-18 wanaodaiwa kujihusisha na matukio ya kuvamia nyumba na kuiba usiku.    Kamanda Sirro alisema watuhumiwa hao wanajulikana kwa jina maarufu la ‘kumi ndani kumi nje’, walikamatwa katika maeneo mbalimbali ya jiji na wanaendelea kuhojiwa na polisi, upelelezi utakapo kamilika watafikishwa mahakamani.    “Watuhumiwa hawa wanavunja milango kwa mawe makubwa na kuiba televishe...