Spika Ndugai Msaidie Rais Magufuli kwa kuzuia walevi wasiingie Bungeni
Kwanza kabisa napenda kumpongeza Rais Magufuli kwa hatua alizochukua dhidi ya aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ya Bwana Kitwanga kwa kwa kosa la ulevi wakati wa kazi, hii imeonyesha dhahiri kuwa Rais Magufuli ni Rais wa anatembea na maneno yake ya kuwa anataka kazi tu na wala si masihala na hana simile na yeyote yule anayeleta mzaha katika kazi bila ya kujali nafasi yake ya kisiasa au ya kijamii Ni Rais asiyetaka mchezo mchezo katika mambo yanayohusu maslahi ya taifa, Magufuli ameonyesha anaweza kufanya zaidi ya watangulizi wake katika kusimamia nidhamu na maadili serikali, ameonyesha asiyetaka uswahiba katika mambo ya uongozi wa nchi. Watanzania kwa ujumla wetu tumsaidie Rais katika kuwatumbua walevi wengine katika maeneo yetu ya kazi pamoja na sehemu zenye huduma za kijamii kama ukienda ofisi unampokuta mlevi haraka sana yafaa kuripoti ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yake. Waheshimiwa kama kitwangwa wapo wengi sehemu za kazi, na hata bungeni tuwatumbue tu bila ya kuwaonea ...