SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 21 Mei 2016

T media news

Spika Ndugai Msaidie Rais Magufuli kwa kuzuia walevi wasiingie Bungeni

Kwanza kabisa napenda kumpongeza Rais Magufuli kwa hatua alizochukua dhidi ya aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ya Bwana Kitwanga kwa kwa kosa la ulevi wakati wa kazi, hii imeonyesha dhahiri kuwa Rais Magufuli ni Rais wa anatembea na maneno yake ya kuwa anataka kazi tu na wala si masihala na hana simile na yeyote yule anayeleta mzaha katika kazi bila ya kujali nafasi yake ya kisiasa au ya kijamii

Ni Rais asiyetaka mchezo mchezo katika mambo yanayohusu maslahi ya taifa, Magufuli ameonyesha anaweza kufanya zaidi ya watangulizi wake katika kusimamia nidhamu na maadili serikali, ameonyesha asiyetaka uswahiba katika mambo ya uongozi wa nchi.

Watanzania kwa ujumla wetu tumsaidie Rais katika kuwatumbua walevi wengine katika maeneo yetu ya kazi pamoja na sehemu zenye huduma za kijamii kama ukienda ofisi unampokuta mlevi haraka sana yafaa kuripoti ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yake.

Waheshimiwa kama kitwangwa wapo wengi sehemu za kazi, na hata bungeni tuwatumbue tu bila ya kuwaonea haya kama alivyofanya Rais Magufuli ili kuwatoa wazembe na wasiowajibika ili nchi yetu isonge mbele.

Natoa rai kwa ofisi ya bunge kuweka vitaa vya utambuzi kwa wanaokunywa pombe na kuingia ndani ya bunge, bunge linapaswa kuhakikisha mheshimiwa yeyote alikunywa pombe asiingie ndani ya bunge na hapo ndipo tutakaa sawa na kudhibiti walevi maeneo ya kazi.

Haiwezikani na si halali hata kidogo waheshimiwa wetu kutufanyia dhihaka ya ulevi ndani ya bunge letu kwa kuingia wakiwa tirarila nia aibu kwa taifa,

Pia nanyi waheshimiwa hebu jiheshimuni na mjipime kwa matendo yenu, haiwezekani tunawalipe, mamilion kwa kodi zetu na magari ya bei mbaya halafu mnatufanyia uhuni haiwekani hata kidogo.

Namuomba Spika Ndugai alisimamie hili la kuhakikisha walevi hawaingii bungeni kwa kufunga vifaa vya utambuzi kwa walevi