Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Viongozi wa Chama cha UDP Watimkia CCK

Viongozi wa Chama cha UDP Watimkia CCK

Picha
Mwenyekiti wa Taifa wa UDP, John Cheyo Viongozi wa Chama cha UDP wamekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Kijamii (CCK), kwa madai kinaongozwa kibabe, hakuna mikutano wala vikao vinavyofanyika ili kukijenga. Viongozi hao ni aliyekuwa mkurugenzi wa uchaguzi wa UDP na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mtwara, Salum Makunganya na Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam na mjumbe wa kamati kuu, Joachim Mwakitiga. Wakizungumza baada ya kukabidhiwa kadi za chama chao kipya jana, viongozi hao walisema UDP imegeuzwa mali ya mtu mmoja ambaye huamua mustakabali wa chama kwa matakwa yake.    Mwakitiga alisema uhai wa chama ni mikutano ambayo inawapa fursa viongozi kujadili na kupanga mikakati ya kukijenga. Alisema jambo la kushangaza kwenye chama hicho mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, John Cheyo haitishi mikutano wala vikao vya ndani.  Makunganya alidai kwa miaka mitano chama hicho hakijaitisha mikutano wala vikao vya kamati kuu na halmashauri kuu ya chama. ...