Jinsi Ya Kumfanya Mwanaume Akupende -Wanaume Watashindwa Kujizuia
Unampenda mwanaume flani lakini hajaonyesha dalili zozote za kukupenda? Umejaribu kutumia maujanja yako uliobarikiwa nayo kama mwanamke lakini bado unashindwa kuinasua akili yake? Kumfanya mwanaume akupende si jambo gumu la kufanya, kile unachohitaji ni kutumia mbinu hakika ambayo imefanyiwa utafiti na kuonyesha kuwa inafanya kazi mia kwa mia. Tukirudia kutumia mbinu hakika ni kuwa kama team ya Nesi Mapenzi, tumekuja na miongozo ambayo ikitumiwa vizuri basi bila shaka unaweza kumfanya mwanaume yeyote akupende. 1. Kuwa machoni mwake Kumfanya mtu akupende ni rahisi. Iwapo mara kwa mara utakuwa machoni mwake itafikia wakati flani kuwa amekuzoea kiasi cha kuwa akienda mahali asipokuona basi hasikii raha. Hii unafaa kuitumia kwa mwanaume unayemzimia kwa kuwa karibu na yeye mara kwa mara. Mfano akienda library kusoma, wewe unafaa uwe uko karibu naye, akiwa ameenda kula lunch katika hoteli flani unaweza kupata kisababu cha kuenda naye nk ilimradi muda wake mwingi awe anakutia machoni. 2....