Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MKUU WA MKOA WA MOROGORO AWATIA NDANI WACHINA WAWILI KWA KUKAIDI AGIZO LA SERIKALI

MKUU WA MKOA WA MOROGORO AWATIA NDANI WACHINA WAWILI KWA KUKAIDI AGIZO LA SERIKALI

Picha
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Steven Kebwe, (katikati) pamoja na ujumbe wake wakifanya ukaguzi wa kushitukiza katika mgodi wa Kiwanda cha Tanzania Zhong Fa Construction Material Group Co Ltd , katika mgodi wa Kiwanda hicho uliopo eneo la Kitongoji cha Mazizi, Kijiji cha Maseyu, Kata ya Gwata, Tarafa ya Mikese, wilaya ya Morogoro, kiwanda hicho kinamilikiwa na wachina, uzalishaji wake ulizuiwa na Serikali kuu tangu mwaka 2010 hadi watakapokamilisha taratibu zote za kisheria zikiwemo na za kimazingira. Mfanyakazi raia wa China, Wang Jun (33) ambaye ni mtunza stoo katika mgodi wa kutengeneza marumaru wa Kiwanda cha Tanzania Zhong Fa Construction Material Group Co Ltd ,kinachomilikiwa na Wachina akiwa chini ya ulinzi wa Polisi kufuatia ukaguzi wa ghafla wa mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Kebwe Steven Kebwe, Aprili 13,2016 akifuatana na ujumbe wa serikali ya mkoa na wilaya ya Morogoro katika mgodi wa Kiwanda hicho uliopo Kitongoji cha Mazizi, Kijiji cha Maseyu, Kata ya Gwata, Tar...