Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA. Taarifa kwa Umma juu ya Uchaguzi wa Meya Jiji la DSM .
Uchaguzi Mkuu ulifanyika tarehe 25.10.2016 na wananchi wa Jiji la DSM Waliamua kuongozwa na UKAWA na ndio maana walichagua Madiwani na Wabunge wengi kutoka UKAWA. Kati ya Majimbo 10 ya Uchaguzi katika Jiji la DSM CCM ilipata Majimbo 3 tu baada ya kuchakachua na UKAWA ilipata yaliyosalia.Hali ni hiyo hiyo kwenye kata .Wananchi Waliamua kuipumzisha CCM kwa kuwa Walikua wamechoshwa na uendeshaji mbaya wa Jiji la DSM . Tangu Uchaguzi umalizike mpaka Leo wananchi wanakosa huduma za Jiji kwa sababu CCM ilitaka kushinda Umeya wa Jiji kwa staili ileile waliyozoea ya goli la mkono. Mara wakaletwa wapiga kura feki kutoka Zanzibar huku Wakijua wazi kuwa TAMISEMI sio jambo la Muungano. Waziri mwenye dhamana na TAMISEMI Mhe. JOHN POMBE MAGUFULI hajawahi kutoa kauli wala kukemea hali hiyo hata siku moja huku akijua wazi kuwa vitendo hivyo vilikua ni kinyume Cha sheria za Nchi. Leo tarehe 26.02.2016 tumeshuhudia Uchaguzi ukiitishwa na baada ya wajumbe Kuwasili wakakutana na kilichoitwa zuio...