Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mbunge wa Ubongo Saed Kubenea Akamatwa na Jeshi la Polisi Leo Asubuhi

Mbunge wa Ubongo Saed Kubenea Akamatwa na Jeshi la Polisi Leo Asubuhi

Picha
MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea amekamatwa na Jeshi la Polisi leo asubuhi wakati akiwa katika Mahakama ya Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, anaandika Faki Sosi. Kubenea amekamatwa na polisi akituhumiwa kushiriki kumpiga Terresia Mmbando, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam. Mmbando alikuwa mwenyekiti wa mkutano wa kumchagua Meya wa Jiji la Dar es Salaam uliofanyika wiki mbili zilizopita na baadaye kuahirishwa hatua ambayo iliibua malumbano. Katika mtandao wa mawasiliano wa mwanahalisi, Kubenea ameandika “leo nikiwa mahakamani Kisutu nimekamatwa na polisi. Natuhumiwa kumpiga Katibu Tawala, nipo polisi kati.” Kubenea ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers alikwenda leo mahakamani kuendelea na kesi yake inayohusu kumtukana Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni. Kesi hiyo ilifunguliwa tarehe 15 Desemba mwaka jana baada ya wawili hao kukutana kwenye Kiwanda cha Nguo cha TOOKU kilichopo Ubungo, jijini Dar es Salaam. Katika tuhuma za k...