Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Chadema Wajifungia Kujadili hatua za kuchukua Dhidi ya Jeshi la Polisi Lililopiga Marufuku Maandamano na Mikutano

Chadema Wajifungia Kujadili hatua za kuchukua Dhidi ya Jeshi la Polisi Lililopiga Marufuku Maandamano na Mikutano

Picha
Viongozi wa Chadema, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Vincent Mashinji jana walijifungia kutwa nzima kujadili hatua za kuchukua dhidi ya kitendo cha Jeshi la Polisi kuzuia maandamano na mikutano ya chama hicho ya kisiasa. Tangu asubuhi jana, viongozi hao walikuwa na kikao katika ukumbi wa Mandela, hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza na wakati wa mapumziko mafupi saa kumi jioni, Mbowe alisema chama hicho kitatoa kauli rasmi leo baada ya kikao kingine kilichotarajiwa kufanyika jana usiku. “Tutatoa kauli rasmi kesho (leo), baada ya vikao. Ninachoweza kuthibitisha ni kwamba tunaendelea kushauriana njia sahihi ya kuchukua,”  alisema Mbowe. Juni 7, mwaka huu polisi ilitangaza kupiga marufuku kwa muda usiojulikana maandamano na mikutano yote ya kisiasa kwa kile kilichodaiwa ni taarifa za kiintelijensia za kuwapo tishio la kiusalama na kuwa wanakwenda kushawishi wananchi kuipinga Serikali. Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwal...