Ukimya Wa Msanii Alikiba Wawatesa Mashabiki Wake Kwenye Mitandao Ya Kijamii
Tupo kwenye ulimwengu ambao mitandao ya kijamii imegeuka kuwa kama chakula ambacho ni lazima ule kila siku. Kwa watu maarufu, mitandao imegeuka kuwa sehemu muhimu kwa wao kuwa karibu na mashabiki wao. Mashabiki wanatarajia kuona kila hatua ambayo msanii anaipitia katika shughuli zake za kila siku. Wanataka kuona si tu picha zake akiwa studio akirekodi muziki au jukwaani akitumbuiza, bali pia za maisha binafsi kama vile akiwa na familia au washkaji. Na kwa mashabiki, msanii wanayempenda akiwa kimya hata kwa siku moja tu, hukosa raha na kila wakati huchungulia kwenye akaunti yake kuangalia nini alichoweka. Kwao ni furaha kuona picha za staa huyo na pindi anapoamua kukaa kimya huwanyima kitu muhimu katika yao. Huo umekuwa ni kama ulevi na unaweza kushangaa kwanini mtu anajiskia hivyo lakini ukweli ni kwamba ‘this is real.’ Mashabiki wa Alikiba wanalalamika kuwa amekuwa kimya sana siku za hivi karibuni. Picha ya mwisho kwenye akaunti yake...