Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya U-SCHOLES WA CARRICK NA UKIMYA WA MANCHESTER UNITED

U-SCHOLES WA CARRICK NA UKIMYA WA MANCHESTER UNITED

Picha
Na Ayoub Hinjo Mara nyingi thamani ya kitu huwezi kuijua hadi pale unapokuwa huna. Ndivyo ilivyo katika dunia yetu sisi wanadamu. Mara moja Xabi Alonso aliporejea Uingereza katika mechi ya kirafiki kati ya Hispania na England alisema kuna jambo linamsikitisha ni jinsi ambavyo makocha wa Uingereza walivyoshindwa kumtumia Michael Carrick katika timu hiyo ya Simba Watatu. “Ni mtu mpole  ambaye kazi yake inaonekana anapokuwa uwanjani. “Nikimwangalia kama najiona mimi, angekuwa Mhispania angepata nafasi sababu ni mtu ambaye anaendana nasi”. Inahitaji akili ya ziada kufahamu alichokielezea Xabi Alonso juu ya Carrick,lazima uwe na ubongo mpana. Wakati Sir Alex Ferguson anamsajili Carrick mwaka 2006 alisema hakika huyu ni kijana mwenye kipaji mwenye bahati ya kucheza Manchester United. Wakati huo huo unaambiwa Arsene Wenger alijaribu kumfatilia zaidi ya miaka miwili ili amsaini katika timu yake ya Arsenal. Kiuhalisia Carrick ni kiungo mshikaji ‘Holding midfiel...