Maneja wa Diamond Sallam Ataja Anapokosea Alikiba, Adai Akitaka Amsimamie yupo Tayari
Meneja wa Diamond, Sallam Sharaff yupo tayari kumsimamia Alikiba iwapo akitaka iwe hivyo. Akiongea kwenye mahojiano na gazeti la Champion, Sallam alisema: Sina tatizo kabisa, akitaka tufanye kazi nitamweleza mahitaji yangu akikubali tutafanya kazi. Nilishawahi kukutana na Kiba, Nairobi, alinifuata akaomba tupige picha, sikuwa na kinyongo, tukapiga ikawa safi japokuwa ile picha aliitumia kunitukanisha baadaye. Akifafanua kuhusu hilo, Sallam alisema: Hakuiweka yeye katika mtandao, aliitoa kwa mashabiki wake ambao wakasema nimeenda Nairobi kumfuata Ne-Yo halafu nikafukuzwa, wakasema mimi ndiyo niliomba kupiga picha na Kiba, ikawa gumzo sehemu nyingi. Ukweli nilikuwa na Ne-Yo na Diamond ambaye alikwenda pale kurekodi, yeye Kiba alikuwa Coke Studio. Anasema Kiba alimuomba radhi na kudai kuwa aliwatumia wapost lakini wakaweka maneno yao. Kuhusu anavyomchukulia Kiba kimuziki, Sallam alisema: Siwezi kusema anakosea wapi, maana kila msanii ana njia zake. Wim...