Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mkurugenzi Mkuu wa Zamani wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Naibu wake wana Kesi ya kujibu

Mkurugenzi Mkuu wa Zamani wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Naibu wake wana Kesi ya kujibu

Picha
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) Ephraimu Mgawe (Kulia) na Makamu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Hamadi Koshuma  *****   Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Ephraim Mgawe na aliyekuwa Naibu wake, Hamad Koshuma wana kesi ya kujibu ya matumizi mabaya ya madaraka, imefahamika. Mgawe na mwenzake wanakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakidaiwa kutumia madaraka yao vibaya kwa kutoa zabuni kwa kampuni ya China ya Communication Construction Company Limited kwa ajili ya ujenzi wa magati katika Bandari ya Dar es Salaam. Jana mahakama hiyo katika uamuzi wake baada ya kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka, iliwaona washtakiwa hao kuwa wana kesi ya kujibu kwa mashtaka yanayaowakabili, hivyo watapanda kizimbani kujitetea, Mei 16 mwaka huu. Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mkazi Cyprian Mkeha anayesikiliza kesi hiyo, alisema kwamba ameridhika kuwa upande wa mashtaka umeweza kujenga kesi dhidi ya washtakiwa ...