NDONDO CUP SASA NI LIVE NDANI YA AZAM TV
Mkuuwa Vipindi wa Clouds Media Shaffih Dauda (kulia) na Mkurugenzi mkuu wa Azam Media Ltd, Rhys Torrington wakikabidhiana mikataba ya makubaliano ya Azam TV kuonesha live michuano ya Ndondo Cup Azam TV imengia makubaliano ya kurusha matangazo ya moja kwa moja Mashindano ya Sports Extra Ndondo Cup msimu huu kupitia channel yake ya Azam Sports HD inayopatikana kwenye vifurushi vyote vya AzamTV. Mashindano ya Sports Extra Ndondo Cup maarufu kama “Ndondo Cup” yanayojumuisha timu 32 yatazinduliwa rasmi tarehe 5/6/2016 Jumapili katika viwanja vya Bandari, Tandika jijini Dar es salaam na kudumu kwa takriban miezi miwili. Mkuuwa Vipindi wa Clouds Media Shaffih Dauda akitia saini mkataba wa makubaliano na Azam TV kuonesha mashindano ya Ndondo Cup msimu huu Mashindano hayo yataanzia katika hatua za makundi na hatimaye kumpata Bingwa ambaye atajinyakulia Tsh. Milioni 10, Mshindiwa pili Milionitano na Mshindi wa tatu Milioni tatu. Mechi ya ufunguzi katika hatua za makundi itakuw...