SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 2 Juni 2016

T media news

NDONDO CUP SASA NI LIVE NDANI YA AZAM TV



Mkuuwa Vipindi wa Clouds Media Shaffih Dauda (kulia) na Mkurugenzi mkuu wa Azam Media Ltd, Rhys Torrington wakikabidhiana mikataba ya makubaliano ya Azam TV kuonesha live michuano ya Ndondo Cup

Azam TV imengia makubaliano ya kurusha matangazo ya moja kwa moja Mashindano ya Sports Extra Ndondo Cup msimu huu kupitia channel yake ya Azam Sports HD inayopatikana kwenye vifurushi vyote vya AzamTV.

Mashindano ya Sports Extra Ndondo Cup maarufu kama “Ndondo Cup” yanayojumuisha timu 32 yatazinduliwa rasmi tarehe 5/6/2016 Jumapili katika viwanja vya Bandari, Tandika jijini Dar es salaam na kudumu kwa takriban miezi miwili.


Mkuuwa Vipindi wa Clouds Media Shaffih Dauda akitia saini mkataba wa makubaliano na Azam TV kuonesha mashindano ya Ndondo Cup msimu huu

Mashindano hayo yataanzia katika hatua za makundi na hatimaye kumpata Bingwa ambaye atajinyakulia Tsh. Milioni 10, Mshindiwa pili Milionitano na Mshindi wa tatu Milioni tatu.

Mechi ya ufunguzi katika hatua za makundi itakuwa itaanza saa 10:00 Jioni na kuruka live ndani ya AzamTV kati ya Mabingwa watetezi wa Ndondo Cup msimu uliyopita FaruJeuri kutoka Vingunguti dhidi ya Temeke Market yaTemeke,Tandika.


Mkurugenzi mkuu wa Azam Media Ltd Rhys Torrington akisaini mkataba wa makubaliano ya kuonesha mechi za michuano ya Sports Extra Ndondo Cup

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Makao Makuuya Azam TV Tanzania, Mkurugenzi mkuu wa Azam Media Ltd, Rhys Torrington amesema kuwa hatua hii ya AzamTV kudhamini Ndondo Cup ni moja kati ya mikakati yake kabambe ya kunyanyua soka la mchangani au soka la mtaani na kutoa fursa kwa wachezaji kuonesha vipaji vyao mbele ya washika dau na mashabiki kwa ujumla katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.

Akasema pia, achezajin wnaweza kutumia nafasi hiyo kama ngazi ya kuwatoa hapo na kuwapeleka katika mashindano ya kitaifa na hatimaye kuchezea klabu kubwa zinazoshiriki ligi daraja la kwanza na Ligikuu nchini Tanzania na kupelekea kutambulika katika soko la kimataifa.


Mkuuwa Vipindi wa Clouds Media Shaffih Dauda akizungumza mbele ya waandishi wa habari

Torrington aliongeza kuwa tokea kuanzishwa kwa Mashindano ya Ndondo Cup misimumi wili iliyopita, AzamTV imeona sasa ni wakati muafaka wa kuhamishia nguvu zake kwenye soka la mchangani kuanzia msimu huu wa tatu wa Ndondo Cup na kwa watazamaji sehemu tofauti kuona “lulu” zilizojificha mtaani.


Shaffih Dauda (kushto) akifurahia jambo na Charles Hilary

Shaffih Dauda Mkuuwa Vipindi wa Clouds Media aliongeze kuwa, walipoanzisha mashindano hayo lengo lilikuwa ni kuthamini soka la mchangani lakini baada ya kuunganisha nguvu na AzamTV ni fursa adimu kwa watazamji kwani watakao ishuhudia Sports Extra Ndondo Cup siyo tu watakaokwenda viwanjani bali ni nchi nzima na hata njeyanchi pia kama ilivyo msemo wa AzamTV “ BurudanikwaWote”.

Kauli mbiu ya Sports Extra Ndondo Cup msimu huu: KampaKampa Tena…