Freeman Mbowe Afunguka Kwa Mara Ya Kwanza Kuhusu Edward Lowassa
Mwenyekiti wa Chadema-Taifa Freeman Mbowe amesema, Edward Lowassa, aliyekuwa mgombea wa chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kuungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), hakutoa hata senti moja alipojiunga na chama hicho. Mbowe amezungumza hayo kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la Chadema linaloendelea hivi sasa Jijini Mwanza. Amesema kuwa, pamoja na kuwepo kwa kauli nyingi kwamba, Lowassa alimwaga pesa kabla ya kujiunga na chama hicho, ukweli unabaki kuwa hakutoa pesa yoyote kama ilivyokuwa ikidaiwa. “Watoto wangu walikuwa wanakula sana maharage, sasa siku moja wakala nyama, jirani akasema umeona Lowassa kaja Chadema,” amesema Mbowe. Akizungumzia migogoro ya kichama iliyokuwa imejitokeza kwenye uchaguzi uliopita Oktoba 25 mwaka huu Mbowe amesema, kuna kila sababu kushughulikia migogoro hiyo kwa haraka. “Migogoro mingi ndani ya Chadema imepelekea kuanguka kwa chama, hivyo itashugulikiwa kwa haraka,” amesema na kuongeza; “U...