Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Arejeshwa Nchini
Balozi Radhia Msuya Rais Dk. John Magufuli, amemrudisha nyumbani aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Radhia Msuya, pamoja na watumishi wengine watano, baada ya muda wao kumalizika. Hii ni mara ya pili kwa Rais Dk. Magufuli kuwarejesha nyumbani Mabalozi wa Tanzania walioko nchi za nje baada ya muda wao wa mkataba kumalizika. Ikumbukwe kuwa Januari 25, mwaka huu, Rais Magufuli alimrejesha nyumbani Balozi wa Tanzania aliyeko London, Uingereza, Peter Kallaghe, kuja kufanya kazi Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Dk. James Msekela na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan, Dk. Batilda Buriani, baada ya mikataba yao kumalizika. Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga, amesema kurudhishwa nyumbani kwa Balozi Msuya, ni jambo la kawaida kwa sababu bado kazi ya kuwarudisha nyumbani Mabalozi waliomaliza mikataba yao linaend...