The Industry Yatambulisha Rasmi Wasanii Wake Mbele ya Waandishi wa Habari leo
THE INDUSTRY MUSIC LABEL TAARIFA KWA UMMA THE INDUSTRY YATAMBULISHA RASMI WASANII WAKE MBELE YA WAANDISHI WA HABARI Kampuni ya Muziki ya The Industry iliyoko chini ya Producer wa Music Nahreel siku ya leo tarehe 6 mwezi wa Tano 2016 imewatambulisha wanamuziki wake watatu wapya ambao watakuwa chini ya usimamizi wa label hiyo. Kati ya wasanii hao watatu wawili ni wake kike ambao ni Rosa Ree na Seline na Wakiume mmoja ajulikanae kwa jina la Wildad The Industry wamesema kazi zao zitaanza kuchezwa redioni na kwenye TV siku si nyingi ambapo jumatatu ijayo wataachia wimbo wa Seline pamoja na Video yake The Industry ni studio na kampuni ya muziki ambayo ipo chini ya kundi la music lenye Mafanikio makubwa la Navy Kenzo ikisimamiwa na Producer Nahreel na msaidizi wake Aika Marealle Wasanii Baadhi Waliokwisha fanya kazi na Studio ya The Industry mpaka sasa toka kuanzishwa kwake hivi karibuni ni Diamond Platnumz na wimbo wake wa Nana, Nikki wa Pili na wimbo wa Baba Swalehe, Joh Makin...