Comoro: jina la rais mtarajiwa mikono mwa wapiga kura 6,000
Mwanamke huyo wa Comoro akiwa mbele ya orodha ya majina ya wagombea katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais Februari 22, 2015 Moroni. AFP/Aboubacar M'CHANGAMA Na RFI Nchini Comoro, wapiga kura 6,300 wanatarajiwa kupiga kura leo Jumatano katika muendelezo wa uchaguzi wa urais ulioitishwa baada ya vurugu wakati wa duru ya pili ya uchaguzi. Kura ya uamuzi wa kuamua kati ya kiongozi wa zamani wa mapinduzi Azali Assoumani na mgombea wa utawala unaomaliza muda wake " Mamadou ". Kanali Assoumani, ambaye aliwahi kuwa rais wa nchi hiyo kuanzia mwaka 1999 hadi 2006, alikua akiongoza katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais wa Aprili 10, kwa 40.98% ya kura, kwa mujibu wa matokeo ya awali. Lakini anamshinda mshindani wake Mohamed Ali Soilihi "Mamadou" kura 2,000 tu sawa na 39.87% ya kura. Duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Comoro ilikubwa na machafuko, hasa katika kisiwa cha Anjouan ambapo masanduku ya kura yaliharibiwa na watu kudhalilishwa katika vituo vya ku...