Kudai Ajira Kwawaponza Wahitimu Wa JKT
WAHITIMU sita wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo kufanya mkusanyiko usio halali na kushawishi wenzao kuandamana kwenda Ikulu kudai ajira, anaandika Faki Sosi. Washtakiwa katika kesi hiyo ni George Mgoba, mwenyekiti wao; Parali Kiwango, makamu mwenyekiti; Linus Steven, katibu wa umoja wa wahitimu hao na wahitimu wengine, Emmanuel Mwasyembe, Ridhiwani Ngowi na Jacob Mang’wita. Akiwasomea mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi, Respicius Mwijage, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Benard Kongola amesema, washitakiwa hao wanadaiwa kwamba 15 Februari 2014 katika eneo la Msimbazi Centre, Ilala Dar es Salaam walipanga njama za kutenda makosa hayo. Katika shitaka lingine watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya mkusanyiko usio halali kwa lengo la kuandamana kwenda kwa Rais kulazimisha kupewa ajira katika utumishi wa umma, jambo ambalo ni kinyume cha sheria na kwamba, hatua hiyo ingesababisha u...