Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Waziri Mkuu: Wataalamu Wa Malikale na uhifadhi wa urithi Kuweni Wabunifu

Waziri Mkuu: Wataalamu Wa Malikale na uhifadhi wa urithi Kuweni Wabunifu

Picha
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wataalamu wa mambo ya malikale na uhifadhi wa urithi asilia (natural heritage) watafute mbinu zitakazoimarisha utunzaji wa rasilmali hizo bila kuathiri mifumo ya uchumi ya nchi zinazoendelea. Ametoa wito huo jana (Jumanne, Mei 31, 2016), wakati akifungua Mkutano wa Kimataifa wa siku nne unaojadili Uhifadhi wa Urithi wa Dunia wa Afrika kama Nyenzo ya kuleta Maendeleo Endelevu ulioanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Arusha (AICC) jijini Arusha. Waziri Mkuu alisema kuna baadhi ya nchi ambazo ni maskini sana lakini zimebarikiwa kuwa na rasilmali kama madini na gesi asilia lakini kwa sababu rasilmali hizo ziko karibu sana na vivutio vya urithi asilia wa dunia, watu wa nchi hizo wanazuiwa kuchuma rasilmali zao ili wasiharibu vivutio hivyo. “Tunatambua umuhimu wa kutunza rasilmali na vivutio vya urithi asilia. Hivi ni kwa nini zisitafutwe teknolojia zinazofaa ambazo zitaruhusu uvunaji wa gesi asilia na madini bila kuathiri uhifadh...