Nape Nnauye Asulubiwa Bungeni ......Wabunge Wamwita ni Waziri Mzigo ( Lumbesa)
Wabunge wamemcharukia Waziri wa Habari, Nape Nnauye kwamba aliwahi kuwaita mawaziri wa Serikali iliyopita mizigo, lakini yeye amezuia matangazo ya moja kwa moja ya Bunge, ili wananchi washindwe kumpima kama ni mzigo au lumbesa. Hayo yalijitokeza jana wakati wabunge walipochangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Habari kwa mwaka 2016/2017, iliyowasilishwa bungeni na Waziri Nape. Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) alieleza kushangazwa na hatua ya Serikali ya Awamu ya Tano kuhimiza wananchi kudai risiti wanaponunua bidhaa, lakini haitaki wananchi waone inavyopanga matumizi yake. Alisema Nape akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, aliwaita baadhi ya mawaziri ni mizigo, lakini amepewa wizara hiyo amezuia mijadala ya wazi ambayo ingesaidia wananchi kumpima. “Nilipoona amepewa wizara ya habari nikajua ataruhusu mijadala ya wazi ili tumuone yeye kuwa hatakuwa mzigo, lakini yeye akawa lumbesa. Hilo amelizuia kwa hiyo tunashindwa kumpima,” alisema. ...