Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Spika Apangua tena Kamati za Bunge

Spika Apangua tena Kamati za Bunge, Wabunge Wapinga

Picha
Spika wa Bunge, Job Ndugai amefanya mabadiliko mengine ya kamati za Bunge kwa kuwaongeza wabunge wapya na kuwahamisha wengine kwenda kwenye kamati nyingine, jambo ambalo limepingwa na baadhi ya wabunge wakidai linapunguza ufanisi. Juzi, Spika Ndugai (pichani) aliwaongeza wabunge wanne wapya walioapishwa bungeni Aprili 19, kwenye kamati za Miundombinu; Ardhi, Maliasili na Utalii; Kilimo, Mifugo na Maji; na Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. Hayo ni mabadiliko ya pili tangu Bunge la 11 lianze rasmi vikao vyake katikati ya Novemba mwaka jana, ikiwa ni kipindi kifupi cha mabadiliko ikilinganishwa na Bunge la Tisa na 10. Katika taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Bunge, mabadiliko hayo yamefanyika kwa mujibu wa kanuni ya 116 (3) na (5) ya Kanuni za Kudumu za Bunge za mwaka 2016, ili kuhakikisha kila mbunge anakuwa mjumbe wa kamati mojawapo ya Bunge.  “Aidha, mabadiliko haya ni kwa ajili ya kuhakikisha kuwa kadri itakavyowezekana, Muundo wa Kamati za Ku...