Neema ya Gesi Yaja ......Wadau Wakutana Kujadili Namna ya Kuanza Mchakato wa Kuchakata Gesi
UJENZI wa Mradi wa Kusindika Gesi (LNG) mkoani Lindi utakaowezesha nchi kuanza kufanya biashara ya gesi nje ya nchi umeanza baada ya jana wadau sita wa mradi huo kukutana na kupeana elimu kabla ya mchakato mzima kuanza wakati wowote mwaka huu. Kwa kutumia mradi huo, Tanzania itaanza kufanya biashara ya gesi kwa kuuza nje ya nchi baada ya kubaini kuwa gesi iliyogundulika baharini inayofikia kiasi cha futi za ujazo trilioni 47, ni nyingi na ikivunwa mahitaji ya ndani hayawezi kuimaliza hivyo kulazimika kuiuza nje ya nchi na kuongezea Taifa mapato. Akizungumza jana katika mkutano wa wawekezaji na serikali kupata elimu ya mradi huo kabla ya kuundwa kwa kamati ya majadiliano ya serikali na kuingia mkataba wa ujenzi, Mkurugenzi wa Utafiti wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kelvin Komba alisema wamekutanisha wadau kutoka serikalini na wawekezaji. Komba alisema mkutano huo ni kuanza taratibu za awali kuwekeza na kuuza gesi kwa kutolewa kitaalamu rasilimali hiyo kwenye vis...