Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo 'Ageuka Mbogo' Baada ya Kukabidhi Zawadi HEWA Mei Mosi
MKUU wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo ameagiza ifikapo leo, wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo, wawe wamewapa zawadi zao watumishi bora wa mwaka huu baada ya kubaini walitoa zawadi hewa kwenye sherehe za Mei Mosi. Ameagiza pia Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Pwani pamoja na mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha, nao kutoa zawadi ya fedha kwa wafanyakazi waliofanya vizuri kwenye vitengo vyao, badala ya kuwapa vyeti pekee. Akizungumza juzi kwenye sherehe za Mei Mosi zilizofanyika kimkoa wilayani Mkuranga, Ndikilo alitoa siku tatu zinazoisha leo, taasisi hizo ziwe zimetekeleza agizo hilo. Alisema walichofanya ni masihara na yeye hayuko tayari kufanyiwa mzaha katika suala hilo, lililoandaliwa kwa muda mrefu. “Katika risala ya Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Mkoa wa Pwani walilalamika kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya waajiri kuwakopa zawadi za fedha watumishi wanaofanya vizuri kama motisha,” alisema. Aliendelea, “Lakini kwa...