MAMA MAGUFULI AMSHUKURU MTUMISHI WA MUNGU TB JOSHUA KWA KUUNGA MKONO JITIHADA ZAKE ZA KUSAIDIA WAZEE
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Baadhi ya Viongozi wa Serikali, Chama na Wazee wakati akiwasili kwenye kituo cha kulea wazee cha Nkaseka kwa ajili ya kutoa misaada ya Chakula, Mavazi pamoja na Vifaa vya Malazi. Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye kituo cha kulea wazee cha Nkaseka Mkoani Mtwara kwa ajili ya kutoa misaada ya Chakula, Mavazi, Madawa pamoja na Vifaa vya Malazi. Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye kituo cha kulea wazee cha Nkaseka Mkoani Mtwara Baadhi ya Wazee walimsikiliza Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli Kaimu Afisa Mfawidhi wa Kituo cha kulea wazee cha Nkaseka Mkoani Mtwara Bw. Rashidi Kambona akimkabidhi taarifa ya kituo hicho Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli. Mke wa ...