Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya SUMATRA Yatangaza Nauli Za Usafiri Wa Mabasi Yaendayo Haraka.

SUMATRA Yatangaza Nauli Za Usafiri Wa Mabasi Yaendayo Haraka.

Picha
Hatimaye  Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imetangaza nauli zitakazo tumika kwa mabasi yaendayo kasi kuwa ni 400, 650 na 800 kwa safari za Mbezi mwisho hadi Kivukoni. Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Giliard Ngewe amesema nauli kutoka Mbezi mwisho hadi Kimara Sh400, na nauli ya Sh650 itatumika maeneo ya  Kimara  kwenda  Kivukoni, Kimara –Kariakoo, Kimara – Morocco, Kariakoo - Kivukoni. Amesema nauli ya Sh800 ni Mbezi Mwisho-Kimara –Kivukoni, kivukoni-Kimara- Mbezi Mwisho, Mbezi Mwisho-Kimara- Kariakoo, Kariakoo-Kimara-Mbezi Mwisho, Mbezi Mwisho Kimara- Morocco,na Morocco- Kimara-Mbezi Mwisho. “Chombo chochote cha usafiri hakitaruhusiwa kutumia barabara za mwendo kasi kuanzia kesho, watakao kiuka agizo watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufutiwa leseni za biashara zao”  amesema. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (S...