Maalim Seif Aendelea Kummwagia Lawama Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Kwa Kupindua Matokeo ya Uchaguzi Mkuu Zanzibar
Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad ameendelea kumtupia lawama Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete akidai kuwa alitumia dola ‘kupindua’ demokrasia ili kuinusuru CCM iliyokuwa imebwagwa kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita. Alisema Kikwete ambaye wakati huo alikuwa Amiri Jeshi Mkuu, anastahili lawama kwa madai kuwa alituma vyombo vya dola kugeuza uamuzi wa Wazanzibari waliokuwa wameufanya kupitia masanduku ya kura Oktoba 25 mwaka jana. Maalim Seif aliyasema hayo jana pale wananchi walipomtaka kutoa neno la kuwasalimu alipopita katika Msikiti wa Ijumaa wa Masjid Swahaba, Mtoni Garagara, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja. “Kilichofanyika si kitendo cha kiungwana hata kidogo, ni uhuni wa hali ya juu uliopangwa kwa makusudi na watu wasioitakia mema Zanzibar na hivyo wakaamua kutoheshimu haki na uamuzi halali wa wananchi,” alisema. Maalim Seif alisema nchi ni mali ya wananchi ambao siku zote watabaki kuwa sehemu muhimu ya uamuzi wa nani awaongoze. Katibu mkuu huyo ambaye alikuwa mgo...