Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya HakiElimu Yashauri Mambo Matano Muhimu Katika Bajeti ya Elimu 2016/2017

HakiElimu Yashauri Mambo Matano Muhimu Katika Bajeti ya Elimu 2016/2017

Picha
Katika kuelekea bunge la bajeti hivi karibuni, serikali imeshauriwa kuongeza bajeti ya sekta ya elimu kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ili kuendana na kauli ya upatikanaji wa elimu bure sambamba na kufidia gharama za uboreshaji na ujenzi wa miundombinu. Kauli hiyo imetolewa jana Jijini Dar es Salaam na John Kalage Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hakielimu, wakati alipokuwa akitoa taarifa ya uchambuzi na ushauri wa Shirika la Hakieli juu ya mwelekeo wa bajeti ya elimu2016/2017. Kalaghe alisema serikali haina budi kuongeza bajeti ya sekta ya elimu kwa mwaka wa fedha 2016/2017 hadi kufikia asilimia 20 ya bajeti ya taifa au asilimia 6 ya pato lote la taiafa. Aidha alisema kwa mujibu wa uchambuzi walioufanya kama shirika, na kwa kuzingatia takwimu za idadi ya wanafunzi, shule na mahitaji, kila mwaka serikali itapaswa kutenga kiasi cha fedha kisichopungua Tsh. bilioni 1,034.5 nje ya mahitaji mengine ya kisekta ili kugharamia elimu bila malipo. “Tunafahamu hivi karibuni bunge linatar...