Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya GUARDIOLA VS MOURINHO: MASWAHIBA WAWILI WALIOGEUKA KUWA MAHASIMU WAKUBWA

GUARDIOLA VS MOURINHO: MASWAHIBA WAWILI WALIOGEUKA KUWA MAHASIMU WAKUBWA

Picha
Na Mahmoud Rajab Naweza kusema vita ama uhasimu unarejea kwa mara nyingine na kunogesha EPL. Tena sio vita vya kawaida maana itakuwa ni vita vya makocha wawili mahasimu na vilabu viwili hasimu. Guardiola atakuwa akiinoa Manchester City msimu ujao wa ligi wakati Jose Mourinho atakuwa akiinoa Manchester United baada ya kumalizana nao kila kitu na kusaini mkataba. Ikumbukwe kwamba, Guardiola na Mourinho wamewahi kufanya kazi pamoja kwa takriban miaka minne wakiwa ndani ya klabu ya FC Barcelona. Wakati huo Guardiola akiwa kama mchezaji na Mourinho akiwa kama kocha msaidizi wa Bobby Robson na baadaye Louis van Gaal. Miaka mingi imeshapita na mengi yametokea. Van Gaal akiwa ameshaondoshwa United na kiti chake kuchukuliwa na Mourinho huku Pellegrini akimaliza muda wake na nafasi yake kuchukuliwa na Pep. Tukirudi miaka mingi nyuma kunako klabu ya Barcelona, Pep na Jose walikuwa ni maswahiba wakubwa. Guardiola, wakati huo akiwa mchezaji alikuwa akiandaliwa kuwa kocha kutokana na uwezo wak...