SIMEONE KATIKA JARIBIO LA MWISHO JANGWANI NA STORI ISIYOELEZEKA
Hakuna kingine anachowaza Diego Simeone wa Atletico Madrid zaidi ya fainali itakayo pigwa kwenye mji wa kihistoria wa Milan nchini Italia. Katika fainali hiyo Diego anaingia akiwa na kisasi cha fainali ya mwaka 2014,Diego anaingia kwenye fainali hii ya sasa akiwa na jeshi kamili huku akiwa amebeba ule msemo unaosema hakuna kitu kitamu kama kisasi “the revenge is sweater than anything”. Nadhani Simeone alikuwa anasali Real Madrid ili afuzu fainali akakutane naye kwa kulipiza kisasi sababu hakuna muda mwingine wa kucheza dhidi yao zaidi ya sasa. Safari ambayo amepitia Simeone kuiwezesha Atletico Madrid kufuzu fainali hii si ya kitoto kabisa. Kuanzia kwenye makundi hadi fainali amecheza na timu ambazo zinachangamoto kubwa na historia kwenye soka la Ulaya. Inahitaji moyo wa chuma kufanikisha hayo yote kama wasemavyo kasi ya kiongozi wa wahuni ndio kasi ya wahuni wenyewe. Moyo mgumu wa Simeone umepandikizwa kwa wachezaji wa Atletico Madrid na yeye mwenyewe Diego. Kumpiga Rea...