Serikali Kuchukua Hatua za Kisheria Kwa Waliofunga Mita za Kupimia Mafuta Bandarini na Kuacha zisifanye Kazi Kwa Miaka Mitano
Kamati ya Miundombinu imeitaka Serikali kuchunguza kwa kina na kuchukua hatua za kisheria kwa yeyote aliyehusika na kufungwa mita za mafuta zilizopo Bandari ya Dar es Salaam, bila kufanya kazi kwa miaka mitano. Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Norman Sigala alisema kuna haja ya Serikali kujiridhisha kwa umakini lengo la kufungwa kwa mita hizo na sababu ya kufungwa kwake, kisha ichukue hatua. “Kamati yetu inatambua wajibu wake ikiwamo kuielekeza Serikali, kuishauri na kuikosoa bila uoga tulitembelea tukaona zile mashine moja ya mafuta ya dizeli tayari ilifungwa na inaendelea kufanya kazi, sasa hiyo nyingine Serikali inapaswa kwenda ndani zaidi kiuchunguzi na kuchukua hatua kali kwa yeyote aliyehusika,” alisema. Februari 12, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifanya ziara ya ghafla kwenye Kitengo cha Upimaji Mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam na kukuta mita zimejaa kutu baada ya kutelekezwa kwa miaka zaidi ya mitano. Kutokana na hali hiyo, alimpa saa ...