Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Samia: Utumbuaji Majipu Serikalini Haumuonei Mtu

Samia: Utumbuaji Majipu Serikalini Haumuonei Mtu

Picha
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema serikali haina nia ya kumwonea mtu, inapochukua hatua ya kutumbua majipu kwa watumishi wa umma. Samia aliyasema hayo juzi baada ya kupokea taarifa ya Mkoa wa Morogoro, iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa huo, Dk Steven Kebwe akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani humo. Alisema lengo la kutumbua majipu ni kurekebisha na kurejesha nidhamu, uadilifu na uwajibikaji serikalini, kama ilivyoangizwa katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili Watanzania wote wafaidike na matunda ya nchi yao. “Mtasikia katika serikali tunarekebisha, majipu yanatumbuliwa... kwa kweli hatuna nia ya kumwonea mtu, tunarekebisha kama ilivyoagizwa katika Ilani yetu ya Chama Cha Mapinduzi ili Watanzania wote wafaidi matunda ya nchi yao,”  alisema Samia. Alisema katika marekebisho hayo, serikali imechukua hatua ya kukata mishahara ya walio juu na kunyanyua ya walio chini waje juu kidogo na kwamba jitihada zote hizo ni katika kufanya mambo yaende ...