Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mkuu Wa Mkoa Wa Mwanza Aagiza Aliyedhulumiwa Kiwanja Arejeshewe

Mkuu Wa Mkoa Wa Mwanza Aagiza Aliyedhulumiwa Kiwanja Arejeshewe

Picha
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ameuagiza uongozi wa Jiji la Mwanza kuhakikisha linakabidhi kiwanja namba 28-A kilichopo katika eneo la Bugando ifikapo Aprili 25, 2016 kwa mmiliki halali wa kiwanja hicho bwana Justine Eminoga ambacho amekuwa akikidai kutoka kwa mfanyabiashara wa Jijini humo kwa zaidi ya miaka sita sasa. Mongella amefikia hatua hiyo mara baada yakupokea malalamiko kutoka kwa bwana Justine ambaye alifika katika Jiji la Mwanza kwa ajili kufatilia suala lake ambalo limedumu kwa zaidi ya miaka sita sasa. Akitoa malalamiko yake mbele ya mkuu huyo wa mkoa, bwana Justine alidai kuzulumiwa kiwanja hicho na mfanyabiashara aliye mtaja kwa jina Shanif Mansour ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kwimba. Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa ametoa siku saba kwa halmashauri za mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanakamilisha zoezi la kuhakiki  watumishi, ili kubaini endapo kuna watumishi hewa waliosalia katika zoezi la awali, zoezi la sasa ambalo linasimamiwa na Ofisi ya katibu ...