Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue Sasa Amestaafu Bila Kupangiwa Kazi Nyingine!
Aliyekuwa Katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue sasa amestaafu bila kupangiwa kazi nyingine kama alivyoahidiwa na Rais John Magufuli siku aliyomteua Balozi Injinia John Kijazi kushika wadhifa huo na hivyo Balozi Sefue kutolewa kwa madai ya kupangiwa kazi nyingine. Tarehe 6 mwezi Machi Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli alimteua John William Kijazi kushika wadhifa wa Katibu Mkuu kiongozi wadhifa ambao hapo kabla ulikuwa ukishikiliwa na Balozi Ombeni Sefue.Balozi Sefue alieteuliwa tena na Rais Magufuli Desemba 20, 2015 kuendelea kushika wadhifa huo kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya utumishi wake wa umma kuisha sambamba na makatibu wakuu na manaibu 50. Katika uteuzi ule wapo makatibu wakuu na manaibu walioachwa akiwemo Dkt.Donald Mbando (Afya),Balozi Liberata Mulamula (Mambo ya Nje), Omari Chambo (Nishati na Madini), Jumanne Sagini(Tamisemi) na Joyce Mapunjo (Afrika ya Mashariki).Balozi Sefue alirudishwa tena lakini ghafla Machi 6 alisimamishwa na ku...