Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MAHREZ AMEUPANDA MLIMA KITONGA KWA MATUMAINI SASA NI WAKATI WAKE KUTULIA KIVULINI

MAHREZ AMEUPANDA MLIMA KITONGA KWA MATUMAINI SASA NI WAKATI WAKE KUTULIA KIVULINI

Picha
Rirad Mahrez amezaliwa February 21, 1991 ni mchezaji wa soka la kulipwa anayekipiga kwenye klabu ya Leicester City ya England na timu ya taifa ya Algeria kama winger. Mahrez alianza soka lake kama mchezaji kijana kwenye klabu ya AAS Sarcelles ya nchini Ufaransa. Mwaka 2009 akaanza rasmi kucheza soka la kulipwa alipojiunga na klabu ya Quimper ambako alichea kwa msimu mmoja pekee na kujiunga na klabu ya Le Havre ambayo aliitumikia kwa miaka mitatu ambapo mwanzo alianza kucheza kwenye kikosi cha wachezaji wa akiba na baadaye kuingia kwenye kikosi cha kwanza na kupata nafasi ya kuanza mara kwa mara. January 2014, Mahrez alijiunga na Leicester City wakati huo ikishiriki ligi daraja la kwanza (Championship) na kukisaidia kikosi hicho kutwaa taji la Football League Championship na kufanikiwa kupanda daraja kucheza Premier League. Mahrez alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa akiwa na Algeria mwaka 2014 na kuiwakilisha nchi yake kwenye fainali za kombe la dunia (FIFA World Cu...