Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Madrid

Listi ya vilabu tajiri duniani, Madrid, Barca zaongoza, Man Utd yaongoza kwa kuingiza faida kubwa

Picha
Mapato makubwa ya fedha zinazotokana na mauzo ya haki za matangazo ya TV , mauzo jezi na mapato ya udhamini wa jezi, wadhamini na ushiriki wa Champions league umeendelea kuzipa uthamani mkubwa vilabu vya soka duniani.     Matokeo yake, wawekezaji ambao waliwekeza kwenye soka katika kipindi cha mika 10 iliyopita sasa wanavuna mapato makubwa hasa katika timu za England.  UEFA imeongeza malipo katika Champions League kwa asilimia 50% kwa miaka 3 kuanzia msimu wa 2015-16. Fainali ya mwaka huu, itakayochezwa San Siro jijini Milan, Italy, baina ya vilabu vya Spain, Real Madrid vs Atletico, kila timu itapata kisi cha $100 million. Mapato ya Champions League msimu uliopita  Vilabu 20 ambavyo vinaongoza kwa uthamani vina thamani ya wastani wa $1.44 billion, ongezeko la 24% kuliko ilivyokuwa miaka 20 iliyopita. Malipo makubwa ya dili za TV, kama mkataba wa miaka wa miaka 3 wenye thamani ya $7.9 billion baina ya English Premier Keague na Sky Sports na BTSport ambao ...

Pamoja na Kiwango Kibovu Uwanjani – Man Utd yazifunika Barca, Madrid, katika listi ya vilabu vyenye faida kubwa

Picha
Mauzo makubwa ya haki ya matangazo ya TV, mauzo ya jezi, mauzo ya wachezaji na uuzaji, matangazo ya biashara na uuzaji wa bidhaa mbalimbali zenye nembo za vilabu ni moja ya mambo yaliyozitengenezea faida kubwa vilabu vya soka kwa muda wa miezi zaidi ya 12 iliyopita.    Jarida la Forbes linalodili na masuala ya biashara na fedha limechapisha listi ya vilabu 10 vilivyoingiza faida kubwa duniani kote.     Pamoja na matokeo yasiyoridhisha uwanjani, klabu ya Manchester United imetajwa na jarida la Forbes la Marekani kuwa klabu iliyoingiza faida kubwa zaidi kwa miezi 12 iliyopita.  Listi kamili ya vilabu 10 vya soka vyenye faida kubwa. 1. Manchester United: $190 million 2. Real Madrid: $162 million 3. Manchester City: $131 million 4. Arsenal: $122 million 5. Liverpool: $115 million 6. Barcelona: $108 million 7. Juventus: $81 million 8. Tottenham Hotspur: $73 million 9. Schalke: $67 million 10. Bayern Munich: $60 million