Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Suarez kuumaliza utawala wa CR7 kwenye PICHICHI? Hizi hapa rekodi alizoweka msimu mpaka sasa

Suarez kuumaliza utawala wa CR7 kwenye PICHICHI? Hizi hapa rekodi alizoweka msimu mpaka sasa

Picha
Luis Suarez yupo njiani kutengeneza historia katika klabu ya FC Barcelona.    Mpaka sasa tayari ametengeneza rekodi ya kuwa mchezaji katika La Liga kufunga magoli manne katika mbili mfululizo. Magoli yake manne dhidi ya Sporting Gijon yanamaanisha mchezaji huyo ameivunja rekodi yake bora ya ufungaji wa magoli ndani ya msimu mmoja. Kwenye msimu huu mpaka sasa, mshambuliaji huyu wa Uruguay ameshafunga jumla ya magoli 53 katika mechi 49. Takwimu zake zinampeleka kwenye kilele cha msimamo wa wafungaji bora kuelekea kutwaa tuzo ya PICHICHI akiwa na magoli 34, magoli matatu zaidi ya CR7 ambaye wikiendi hii hakucheza, magoli yake 8 katika mechi mbili zilizopita yamemrudisha kwenye kinyang’anyiro cha kugombea kiatu cha dhahabu cha UEFA.    Mpaka sasa, msimu wake bora kabisa ulikuwa msimu wa 2009-10, alipokuwa akicheza Ajax. Msimu huo alifunga jumla ya magoli 49 katika mechi 48, kiasi cha magoli ambacho alikifikia wakati Barca walipoifunga 8-0 Deportivo la Coruna ka...