NSSF Haina Mkurugenzi wala Kaimu kwa Wiki Mbili Sasa
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linamaliza siku ya 15 likiwa halina kiongozi baada ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu, Dk Ramadhan Dau kuteuliwa kuwa balozi na kuacha mara moja shughuli za kila siku za taasisi hiyo kubwa, hali iliyofanya shughuli zake kudorora. Rais John Magufuli alimteua Dk Dau kuwa balozi Februari 15, sambamba na makada wengine wawili wa CCM, Dk Asha Rose Migiro na Mathias Chikawe, akisema vituo vyao vya kazi vitajulikana baada ya taratibu za kidiplomasia kukamilika. Tangu wakati huo, NSSF imekuwa ikijiendesha bila ya kiongozi mkuu na habari kutoka ndani ya shirika hilo zinasema kuwa shughuli za shirika hilo kubwa kuliko yote yanayojihusisha na hifadhi ya jamii nchini, haziendi kutokana na kutokuwapo na mtu aliyepewa jukumu la kukaimu nafasi hiyo. Miongoni mwa mambo hayo ni ufunguzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam ambalo lilitakiwa lianze rasmi kutumika Machi Mosi, ununuzi wa magari ya ofisi za mikoa, mkutano wa wanachama wa mwaka pamoja na wiki...