MNYAMA AENDELEA KUTAMBA VPL, KIIZA AREJEA KWENYE RELI
‘Wekundu wa Msimbazi’ Simba wameendelea kufanya vizuri kwenye ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kufuatia ushindi mnono wa magoli 3-0 dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara kwenye mchezo wao wa marudiano uliochezwa kwenye uwanja wa taifa. Simba ilianza kupata bao la kwanza lililofungwa na Mwinyi Kazimoto dakika ya 32 akiunganisha vizuri krosi ya Ibrahim Ajib. Dakika ya 52 Kiiza angafunga bao la pili ambalo lilikuwa ni bao lake la 17 kwenye ligi, Kiiza aliunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Ibrahim Ajib. Kiiza aliifungia Simba bao la tatu na kuchukua usukani wa wafungaji bora wa VPL baada ya kuunganisha pasi ya Danny Lyanga aliyeuwahi mpira uliotemwa na golikipa wa Ndanda kufuatia shuti kali la mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Justice Majabvi. Simba imefikisha jumla ya pointi 51 baada ya kucheza michezo 22 na kurudi kileleni mwa ligi kwa mara nyingine wakiitoa Yanga yenye pointi 50 ikiwa imecheza michezo 21. Takwimu muhimu unazotakiwa kuzifahamu Simba wameifunga Nda...