SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 10 Machi 2016

T media news

MNYAMA AENDELEA KUTAMBA VPL, KIIZA AREJEA KWENYE RELI



‘Wekundu wa Msimbazi’ Simba wameendelea kufanya vizuri kwenye ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kufuatia ushindi mnono wa magoli 3-0 dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara kwenye mchezo wao wa marudiano uliochezwa kwenye uwanja wa taifa.

Simba ilianza kupata bao la kwanza lililofungwa na Mwinyi Kazimoto dakika ya 32 akiunganisha vizuri krosi ya Ibrahim Ajib.

Dakika ya 52 Kiiza angafunga bao la pili ambalo lilikuwa ni bao lake la 17 kwenye ligi, Kiiza aliunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Ibrahim Ajib.

Kiiza aliifungia Simba bao la tatu na kuchukua usukani wa wafungaji bora wa VPL baada ya kuunganisha pasi ya Danny Lyanga aliyeuwahi mpira uliotemwa na golikipa wa Ndanda kufuatia shuti kali la mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Justice Majabvi.

Simba imefikisha jumla ya pointi 51 baada ya kucheza michezo 22 na kurudi kileleni mwa ligi kwa mara nyingine wakiitoa Yanga yenye pointi 50 ikiwa imecheza michezo 21.

Takwimu muhimu unazotakiwa kuzifahamu

Simba wameifunga Ndanda FC mara zote walizokutana tangu timu hiyo ya Mtwara ilipopanda daraja kucheza ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2014-2015.
Ndanda haijawahi kufunga goli hata moja mbele ya Simba, mara zote imekuwa ikifungwa bila yenyewe kupata goli. January 17, 2015 (Ndanda 0-2 Simba), April 25, 2015 (Simba 3-0 Ndanda), January 8, 2016 (Ndanda 0-1 Simba) na March 10, 2016 (Simba 3-0 Ndanda)
Ibrahim Ajib amehusika kwenye magoli mawili ya leo. Alipiga krosi kwa Mwinyi Kazimoto ambaye akafunga bao la kwanza kisha kona yake ikatua kichwani kwa Hamisi Kiiza aliyeandika bao la pili.
Kiiza amefikisha mabao 18 baada ya kufunga bao mbili kwenye mchezo kati ya Simba dhidi ya Ndanda FC. Kiiza anamzidi Amis Tambwe wa Yanga mwenye mabao 17 aliyofikisha baada ya kufunga magoli mawili wakati Yanga iliposhinda kwa magoli 5-0 dhidi African Sports.
Simba imeifunga Ndanda magoli 3-0 kwa mara ya pili ndani ya mechi mbili walizokutana kwenye uwanja wa taifa. Mara ya kwanza ilikuwa ni April 25, 2015 (Simba 3-0