SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 10 Machi 2016

T media news

Waliokufa baada ya kuporomoka jengo Nigeria ni 30

Idadi ya waliopoteza maisha baada ya jengo lenye ghorofa 5 kuporomoka katika mji mkuu wa kibiashara wa Nigeria, Lagos imepindukia 30.Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nigeria imesema kuwa, jengo hilo ambalo lilikuwa linaendelea kujengwa liliporomoka Jumanne iliyopita, kutokana na ukiukaji wa kanuni za ujenzi. Imesema kuwa, jengo hilo liliporomoka baada ya mmiliki wake kuamua kuongeza ghorofa za ziada pasina idhini ya mamlaka husika. Awali iliripotiwa kuwa watu 4 tu ndio waliokuwa wameaga dunia katika mkasa huo lakini kufikia jana jioni baada ya shughuli za kupekua vifusi kukamilika, miili zaidi ilipatikana.Aidha watu 13 walipatikana wakiwa hai katika shughuli hizo jana Jumatano. Taarifa hiyo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nigeria imemtaka mmiliki wa jengo hilo kupiga ripoti mara moja katika kituo chochote cha polisi la sivyo mkono wa sheria utafuata mkondo wake.