SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 29 Machi 2016

T media news

UN: Wanawake washirikishwe katika juhudi za kuleta amani barani Afrika


UN: Wanawake washirikishwe katika juhudi za kuleta amani barani Afrika
Umoja wa Mataifa umesisitizia umuhimu wa kupewa nafasi zaidi wanawake wa bara la Afrika kwa ajili ya maendeleo ya kijami na kisiasa kwa lengo la kuimarisha usalama na uthabiti barani humo.
Hayo yamesemwa na Phumzile Mlambo-Ngcuka, mratibu wa masuala ya wanawake katika umoja huo katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambapo aliitaka jumuiya ya kimataifa kuunga mkono suala la wanawake kutokana na nafasi yao katika kudumisha amani katika jamii. Amesema kuwa, pamoja na nafasi chanya waliyonayo wanawake katika suala zima la kudumisha amani, lakini wamekuwa wakinyimwa fursa za ushiriki wao katika maendeleo. Bi. Phumzile Mlambo-Ngcuka ameashiria suala la kuanzishwa vituo vya kutatua migogoro ambavyo vinasimamiwa na wanawake kwa ajili kusimamia chaguzi na masuala mengine ambapo vimekuwa na mafanikio makubwa. Mratibu wa masuala ya wanawake wa Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa, hata katika mazungumzo na viongozi wa vyama vya kisiasa au viongozi wa usalama katika nchi zenye migogoro, utendaji wa wanawake umeonekana kuwa na natija chanya suala ambalo linathibitisha nafasi yao muhimu katika jamii.