SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 29 Machi 2016

T media news

Namna ya kuondoa Asidi inayosababisha Kiungulia katika Maharage.


Maharage ni moja ya vyakula ambavyo mimi hukwepa kula nje ya nyumbani ,naweza kula maharage nje ya nyumbani kwangu endapo tu ninauakika na ambavyo mpishi kaandaa maharage hayo,kwa maana nyingine nakula kama yameandaliwa na ndugu,jamaa na marafiki ambao ninauhakika na uandaaji wao.
Hii yote ni kwasababu maharage yasipoandaliwa vizuri hunipa kiungulia kikali sana kwa muda mrefu na wakati mwingine tumbo hujaa gesi na kuninyima raha.
Maharage ni chanzo kizuri cha protini daraja B(protini itokanayo na mimea)na Nyuzinyuzi.
Asidi aina ya Phytic au phytates ipatikanayo kwenye maharage ikutanapo na madini mwili kama zinc,copper,calcium,magnesium namadini chuma husababisha tatizo la kiungulia na tumbo kujaa gesi kwa baadhi ya watu,tatizo hili huwasumbua zaidi wale wasiokula Nyama na vyakula vitokanavyo na wanyama(vegeterians)kwani vyakula vyao hua na aside nyingi ya phytic.
Tafiti zilizofanywa na American Dietetic Association zinaonyesha kwamba huwezi toa aside yote ya phytic kwenye maharage ila unaweza kuipunguza kwa kiasi kikubwa kwa kuloweka maharage kwenye maji.
Wengi mnaloweka maharage kwenye maji ili kuyalainisha na kufanya yaive haraka wakati wakupika,Lakini msichojua ni kwamba kuloweka huko hupunguza aside ya Hyptic kwenye maharage ambayo ni chanzo cha kiungulia kwa wengi,aside hiyo pia hutonesha vidonda vya tumbo na kuleta maumivu makali kwa wale wenye tatizo la vidonda vya tumbo.
Ulowekaji wa maharage kwa muda mrefu
Watu wengi wamezoea kuloweka maharage usiku na kuyapika siku inayofatia,ikimaanisha yanalowekwa kati ya masaa manane hadi kumi na nane.
Ingawa kuloweka huku kumezoeleka kwa wengi.Tafiti zinaonyesha kwamba,njia hii ya ulowekaji wa maharage ni hatari sana kwa afya kwani hutoa nafasi, mazingira sahihi na muda mrefu kwa vijidudu viletavyo magonjwa vipatikanavyo kwenye maharage kuzaliana na kukua .
Ingawa maharage hupikwa kwa muda mrefu na kwa moto mkali bado haitoshi kuuwa vijidudu vya aina yote,bakteria watengenezao sumu au spore mara nyingi hubakia hai na huweza kua chanzo cha magonjwa kwa mlaji wa maharage hayo.
Ukiamua kutumia njia hii,basi loweka maharage na uyaweke ndani ya friji ili kupunguza uwezekano wa vijidudu hao kuzaliana kwenye maharage.
Ulowekaji wa maharage kwa muda mfupi-Njia iliyo bora
Kuloweka maharage kwa muda mfupi ni njia nzuri na bora zaidi ya kupunguza asidi ya phytic kwenye maharage,kwani huipunguza kwa kiwango kikubwa na kwa haraka zaidi kuliko njia ya kuloweka maharage kwa muda mrefu.
Njia hii fupi kwa upande mwingine haitoi nasafasi ya vijidudu viletavyo magonjwa kuzaliana kwenye maharage,na huokoa muda kwani huchukua muda mfupi.
Ulowekaji huu huchukua kati ya saa moja adi manne na si zaidi,ni uamuzi wa mpishi kuchagua aloweke masaa mangapi,ata hivyo ni vyema kujua kwamba ukiloweka kwa masaa manne utatoa kiasi kikubwa cha phytic kuliko ukiloweka kwa saa moja.
Njia.
1.Pima kiasi cha maharage unachotaka kuandaa/kupika,mfano:vikombe vinne.(nashauri utumie kikombe kupima)kariri idadi ya vikombe ulivyopima
2.Chambua maharage ili kuondoa maharage mabovu,mawe na uchafu mwingine wowote

3.Osha maharage hadi yawe safi.

4.Kwa kutumia kikombe ulichopimia maharage ,pima maji mara mbili ya kipimo cha maharage na uweke kando.mfano:kwakua tumepima maharage vikombe vinne,tutapima maji vikombe nane.(vikombe vya maji,mara mbili ya vikombe vya maharage)

5.Katika sufuria weka maharage na kisha ongeza maji uliyopima

6.Bandika maharage jikoni yachemke kwa dakika mbili tu.Esabu dakika mbili kuanzia pale yanapoanza kutokota na sio dakika mbili kuanzia ulipoyabandika jikoni.Epua jikoni baada ya dakika hizo kuisha.

7.Acha kwa kati ya saa moja adi manne(kutokana na muda ulionao)
Muonekano wa maharage baada ya masaa manne
Muonekano wa maharage baada ya masaa manne
8.Chuja maji yote kwenye maharage.

Maji yaliyochujwa kwenye maharage.maji haya yamebeba phytic iliyotoka kwenye maharage.
Maji yaliyochujwa kwenye maharage.maji haya yamebeba phytic iliyotoka kwenye maharage.
9.weka maharage kwenye sufuria, ongeza maji ,bandika jikoni kisha chemsha adi maharage yaive.
Maharage yaliyoiva,baada ya kuchemshwa
Maharage yaliyoiva,baada ya kuchemshwa
Baada ya kuivisha maharage ,unaweza kuyapika au kuyaunga katika namna upendayo.
Maelezo ya ziada.
Ingawa njia hii hupunguza phytic kwa kiasi kikubwa sana na hutosha kufanya mtu asipate kiungulia au tumbo kujaa gesi,kuna wale wenzangu ambao hata iyo hyptic kidogo sana iliyobaki kwenye maharage inatosha kuwapa kiungulia.
Ipo namna ya kukata nguvu ya hiyo phytic kidogo iliyobaki na kufanya maharage yawe mazuri zaidi.