SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 30 Machi 2016

T media news

Kikao cha ushirikiano wa nchi za Mashariki mwa Afrika chaendelea nchini Burundi


Kikao cha ushirikiano wa nchi za Mashariki mwa Afrika chaendelea nchini Burundi
Kikao cha ushirikiano na ustawi wa kijamii wa nchi za ukanda wa eneo la Mashariki mwa Afrika, kinaendelea jijini Bujumbura, Burundi licha ya mgogoro wa kisiasa kuendelea kushuhudiwa nchini.
Kikao hicho ambacho ni cha nne kati ya makongamano ya viongozi wa nchi za eneo la Mashariki mwa Afrika, kilianza jana Jumanne mjini Bujumbura. Katika ufunguzi wa kikao hicho, Joseph Butore Makamu wa Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo alisema kuwa, kufanyika kikao hicho kwa kuhudhuriwa na viongozi wa kieneo, ni kwa lengo la kuanzisha ushirikiano wa pamoja katika masuala ya kisiasa kieneo. Butore aliongeza kuwa, kueneza ustawi wa kijamii na kiuchumi kupitia njia ya ushirikiano wa serikali kuu, ni miongoni mwa malengo makuu ya kikao hicho cha siku mbili. Amesema kuwa, ni suala lisilo na shaka kwamba, kuimarishwa ushirikiano wa nchi za eneo kunaweza kuboresha juhudi za kukabiliana na umasikini na kuboresha maisha ya raia wa nchi hizo za Mashariki mwa Afrika. Nchi za Mashariki mwa Afrika, zinajumuisha Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda, Tanzania, Eritrea, Ethiopia, Djibouti, visiwa vya Ushelisheli, Comoro, Somalia, Sudani Kusini na Mauritius.