Mchungaji Gwajima Afunguka..Ampa Sifa Magufuli..Adai Adai Mafisadi wa Awamu ya Nne Ndio Wanafanya Jitihada za Kumkwamisha
Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema mafisadi walioinyonya nchi katika Serikali ya awamu ya nne, ndiyo wanaoona utawala wa Rais John Magufuli haufai. Akizungumza masuala ya kitaifa kwa kifupi, huku akitoa mafundisho kwa waumini wake jana katika ibada kanisani kwake, Gwajima alimtaka Dk Magufuli aendelee kushikilia uzi huo huo bila kuulegeza. Gwajima ambaye mwaka jana, wakati wa vuguvugu za kampeni ya Uchaguzi Mkuu, aliwahi kusema wasiopenda kuona yeye akimsaidia aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa basi wachukue ndimu wale, jana alisema mafisadi ni wachache na Magufuli anafanya kazi ili kuhakikisha Watanzania wengi wananufaika na uongozi wake. Mara kadhaa, Askofu Gwajima alikaririwa akisema kuwa atamsaidia kiongozi yeyote mwenye lengo la kuleta mabadiliko ya taifa, bila kujali anatoka chama gani. Katika mikutano yake, Gwajima alikuwa akiwataka waumini wake kuchagua kiongozi wanayedhani atawaletea ...