Lowassa Ajisafisha Tuhuma za Kukwapua ardhi Ya Wananchi na Kujimilikisha
Siku chache baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kulieleza Bunge kuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alijimilikisha shamba la Makuyuni Wilayani Monduli mkoani Arusha, Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga amejitokeza kutoa ufafanuzi unaomsafisha. Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Kalanga alisema kuwa Lowassa hamiliki shamba hilo la Makuyuni kwakuwa tangu Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa alipofuta hati ya umiliki wa shamba hilo kutoka kwa raia wa Kigeni aliyemtaja kwa jina la Stein, bado halijamilikishwa rasmi kwa wananchi na ndio ilikuwa hoja yake. Alisema kuwa maelezo ya Lukuvi hayakuwa na ukweli na kwamba alichanganya kati ya shamba hilo la Mkuyuni na shamba la Manyara Ranchi ambalo hati yake ilifutwa tangu mwaka 2000 na kukagawiwa kwa wananchi wa Monduli ambapo Lowassa alisaini hati miliki yake kama muwakilishi wa wananchi wa Wilaya hiyo kwakuwa wakati huo alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya udhamini...