Chadema Yaunda Chombo Kipya Cha Kulisimamia Jiji la Dar es Salaam
Katika kile kinachoonekana kutaka kuliongoza Jiji la Dar es Salaam kwa mafanikio ya kupigiwa mfano, Chadema imeunda chombo kipya cha uongozi katika jiji hilo na kukiita ‘Uongozi wa Dar es Salaam Kuu’. Pia, imemteua Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara kuwa mwenyekiti wa chombo hicho. Chama hicho kikuu cha upinzani nchini kimeunda chombo hicho, huku kikieleza kuwa na uhakika wa kushinda uchaguzi wa meya wa jiji hilo kwa ushirikiano na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutokana na kuwa na idadi kubwa ya madiwani ikilinganishwa na CCM. Uchaguzi huo umeahirishwa mara tatu na ya mwisho kwa kutumia zuio ‘batili’ la Mahakama na kuzua mtafaruku kati ya wabunge na wadiwani wa chama hicho dhidi ya polisi, jambo lililosababisha wabunge wawili, Halima Mdee na Waitara pamoja na madiwani watatu kufikishwa mahakamani wakidaiwa kumshambulia Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo. Akizungumza na waandi...