Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Ataka Mamlaka za Uteuzi Ziwaondoe

Vigogo Jiji la Dar es Salaam Wakalia Kuti Kavu....Makonda Afichua Siri Mikataba Tata, Ataka Mamlaka za Uteuzi Ziwaondoe

Picha
Kamati maalumu ya uchunguzi iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda imefichua madudu na harufu ya ufisadi katika utekelezwaji wa mikataba mitatu, inayohusu maeneo ya ukusanyaji mapato ya Stendi Kuu ya Mabasi Yaendayo Mikoani ya Ubungo na kodi ya uegeshaji magari katikati ya mji. Kutokana na madudu hayo, Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha wazi kuwa hataki kufanya kazi tena na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe na Kaimu wake, Sarah Yohana na kuwasilisha majina yao kwa mamlaka husika ya nidhamu kwa hatua zaidi. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, alisema hivi karibuni aliunda kamati hiyo maalumu kufuatilia maeneo hayo muhimu kutokana na malalamiko ya muda mrefu, ambayo ofisi yake ilikuwa ikipokea kutoka kwa wananchi. Alisema kwa mujibu wa uchunguzi, kamati hiyo ilibaini kuwa katika stendi ya mabasi ya Ubungo, kumekuwa na ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma, ikiwemo kutokuwasilishwa kwa mapato halisi yanayotokana na makusanyo ya kila siku ...